Jumatatu , 2nd Sep , 2019

Staa wa BongoFleva Ali Kiba "King Kiba" amefunguka kuhusu mshikimano wa kazi sanaa na kufanikiwa kutenganisha ustaa wake na familia katika maisha.

Alikiba

Staa huyo ameyazungumza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, kuhusu umoja wa suala la sanaa kwa Bongo Movie.

"Sanaa ni kitu ambacho kinapendeza sana, tunaishi kwenye sanaa kwa muda mwingi ukisikiliza muziki unaishi kwenye sanaa, ukienda 'salon' kunyoa au kusukwa na kujiremba ni sanaa hata ukivaa nguo nzuri za mitindo ni sanaa pia", amesema.

Alikiba ameendelea kusema sanaa ina upana mkubwa na amesisitiza kama wanasanaa watakubaliana kuwa na mshikamano watafika mbali ila kuna mgawanyiko ambao hauleti maana na wakikaa  pamoja watafanya jambo kubwa.

Aidha Ali Kiba ameeleza kitu alichofanikiwa kutenganisha kuishi katika ustaa na familia katika maisha.

"Ni kwa sababu tunaishi maisha ambayo ni ya ukweli. Mimi naishi kama watu wengine wanavyoishi, siishi kistaa na nikisema niishi kistaa watu wataniogopa kwa sababu naweza kuishi hivyo. Ila sitaki kwa sababu nafurahia maisha ambayo nayaishi".

Pia amesema haoni sababu ya kuishi hivyo kwa kuwa hakuna mtu anayeijua kesho yake na anataka kuishi kwa usawa na kujiheshimu sana.