Jumanne , 24th Aug , 2021

Mchekeshaji Annastazia Exavery 'Ebitoke' amemtaja Alikiba kwamba ndio msanii anayeilinda heshima ya muziki wa BongoFleva.

Picha ya mchekeshaji Ebitoke na Alikiba

Kupitia page yake ya Instagram Ebitoke amepost video ya Alikiba akiimba remix ya wimbo wa songi songi ya msanii Maud Elka.

"King  ni mmoja tu wa Bongofleva wengine endeleeni kuimba Amapiano zenu, huyu ndio mfalme anayetulindia Bongofleva yetu

Hii ni mara ya pili kwa mchekeshaji Ebitoke kueleza hisia zake juu ya kumkubali Alikiba wiki moja iliyopita alishea picha ya msanii huyo akieleza kuwa amemuota ndotoni.