Alikiba na Yvonne Chakachaka waomba msaada

Alhamisi , 6th Dec , 2018

Mkali wa muziki wa Bongofleva Alikiba amesisitiza uwepo wa tamasha lake la kufunga mwaka ambalo atashirikiana na msanii kutoka Afrika Kusini Yvonne Chakachaka huku akiwaomba amshabiki kumpangia ngoma za kuimba siku hiyo.

Yvonne Chakachaka na Alikiba

Alikiba ambaye ameshaweka wazi kuwa atafunga mwaka kwa kuwa na tamasha la 'Funga Mwaka na KingKiba', leo amethibitisha kuwa amekutana na Yvonne Chakachaka kwaajili ya maandalizi ya awali ya tamasha hilo.

''Show ya kwanza nipo hapa na Mama Yvonne Chakachaka, tunafanya 'set list'. Ungependa tuimbe nyimbo gani siku hiyo ya tarehe 22 December'', ? amewauliza mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Novemba 29, 2018 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa, msani huyo aliitumia kutangaza ujio wa matamasha mawili ya kufunga mwaka ambayo yote yatafanyika jijini Dar es salaam Desemba 22 na 29.