Jumanne , 20th Feb , 2018

Anaitwa Andrew Clement G. Serkis ambaye alizaliwa April 20, 1964, huko London Uingereza, akiwa mtoto kwenye familia yenye watoto wanne. Mama yake alikuwa ni mwalimu wa shule za watu maalum na Baba yake alikuwa ni daktari.

Akiwa mdogo Andy alipenda kuwa msanii, alikuwa akichora na kuigiza mwenyewe. Akiwa chuo Andy aliombwa kuigiza kwenye 'play', na kuamua kutoka kwenye uigizaji wa jukwaani mpaka kwenye filamu.

Mwaka 1999 Andy alipata bonge la zali la kuigiza kwenye filamu ya The Lord of the Rings" kama kibwengo Gullam, na kumpatia umaarufu mkubwa zaidi na kuwa filamu pendwa, hukuikijitwalia tuzo za Oscar 11.

Alipopata didli la kuigiza filamu ya King Kong kama King Kong mwenywe, Andy alisema kuwa ilimpasa kuja Afrika Mashariki nchini Rwanda na kukaa msituni, kujifunza tabia za sokwe kabla hajaanza kushoot filamu hiyo, jambo ambalo halikumpa ugumu hata alipopata dili la kuigiza kwenye baadhi ya filamu za Planet of the Appes kama 'King Caesar', kwani alishakuwa na uzoefu mkubwa.

Huyo ndiye Andy Serkis, muigizaji aliyecheza filamu mbali mbali kali na watu wengi kuvutiwa na uhusiak wake.

Gollum kwenye Lord of the Rings
King Caesar kwenye Planet of the Apes
King Kong