Jumatatu , 9th Feb , 2015

Msanii wa muziki kutoka Benin Angelique Kidjo amesema kuwa tuzo ya Grammys aliyoipata ni heshima kubwa kwake inakuwa ni maalum kwa ajili ya wanawake wa Afrika.

Mwanamuziki nyota kutoka Benin Afrika, Angelique Kidjo

Msanii mkubwa wa muziki kutoka Benin Afrika, Angelique Kidjo ambaye amefanikiwa kushinda tuzo kubwa ya Grammys katika kipengele cha Best World Music Album, Angelique amesema kuwa tuzo hii ya heshima kubwa kwake inakuwa ni maalum kwa ajili ya wanawake wa Afrika.

Kidjo katika maneno yake ya shukrani amesema kuwa, kwa upande wake muziki ni silaha ya Amani akuwa anaamini kuwa katika dunia ya sasa wasanii wana nafasi kubwa ya kusimamia uimara wa dunia.

Msanii huyu anashinda tuzo hii kubwa kwa mara ya pili sasa, ikikumbukwa pia kuwa mwaka 2007 alishinda kwa mara nyingine kupitia albam yake inayosimama kwa jina Djin Djin.