Aslay afiwa na mama mzazi

Jumamosi , 12th Sep , 2015

Kundi la Yamoto Band, familia nzima ya TMK Wanaume Family chini ya Mkubwa na Wanawe wamepata pigo kubwa baada ya msanii Aslay Isihaka kufiwa na mama yake mzazi aliyekuwa anasumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na Kisukari.

Aslay

Kifo cha mama wa msanii huyo kimetokea leo alfajiri katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Meneja wa msanii huyo, Said Fella kwa masikitiko leo ameongea na eNewz kuifahamisha Afrika Mashariki kuhusiana na tukio hilo la huzuni, na kuweka wazi kuwa kwa sasa msiba upo Temeke, taratibu zikiendelea kuweka na baadhi ya ndugu wakisubiriwa kufika kukamilisha taratibu, tayari kwa maziko ambayo yameadhimiwa kufanyika kesho.

Vilevile eNewz tukapata nafasi ya kipekee ya kuzungumza na Aslay pia, ambaye anaendelea kukubaliana na hali halisi ambapo alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na kifo cha mama yake kipenzi, akiahidi kuweka wazi picha halisi ya pengo la mama yake na namna familia itakavyobaki baada ya msiba.

Sauti ya Said Fella (Juu) Picha ya Mama Aslay (R.I.P)
Sauti ya Aslay (Juu), Picha ya Meneja Said Fella