Jumanne , 5th Jan , 2016

Staa wa muziki AT, amezikandia jitihada zilizoanza kuchukuliwa kusimamia wasanii wa muziki kutoka Tanzania visiwani, kauli yake ikihusishwa na hatua ya msimamizi maarufu wa muziki hapa nchini, Said Fella kuchukua wasanii Baby J na Berry Black.

Staa wa muziki kutoka Zanzibar AT

AT ambaye ameonyesha dhahiri kutokufurahishwa na mfumo wa muziki hapa Tanzania ambao kwa upande wake anaona unabana wasanii wa muziki kutoka Zanzibar, kauli aliyoibua kutoka katika mahojiano yake na Planet Bongo, amesema jitihada hizo zinazofanyika kusimamia wasanii wa visiwani ni kung'ong'a na si kuwasaidia.