
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Akizungumza na 'Big Chawa' kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Waziri Mwakyembe amesema alipotoa kauli hiyo watu walipokea vibaya, kutokana na elimu ndogo na uelewa wao mdogo, hivyo wakaamua kuacha hivyo walivyoelewa, huku akisema wasanii wanatakiwa wajikite katika kupigania haki zao kwani wao bado masikini.
"Ni kwa ajili ya elimu, elimu ndogo lazima huwezi kuelewa, kwa sababu ukiongea kitu 'out of context' ukakijadili hutakuja kukielewa milele, hilo suala limeongelewa bungeni nyie huku mkalichukua vingine kabisa, basi tunawaacha poteleeni mbali, Mbunge wa CHADEMA alisema sisi tuwatelekeza hawa vijana, na mimi nikageuza nikasema mnawatumia vijana vibaya, nimekuja hapa nyie piganieni haki yenu, nyie ni masikini mnahitaji haki, nyie baada ya kupigania haki mnashikilia hoja za kitoto, basi tu ubabaishaji".
Msikilize hapa akiongea na Big Chawa, umsikie alivyofunguka akiwachana wasanii kujihusisha na siasa.