
Ommy Dimpoz
Ommy amefunguka hayo kwenye 'story' tatu ya Planet Bongo ndani ya East Africa radio na kusema kuwa wasanii mkubwa wanapotafutwa na msanii mdogo kwa ajili ya kazi mara nyingi hujivalisha u-bize wasiokuwa nao kwa sababu tu tayari ni staa.
"Msanii mkubwa ni mkubwa tuu, kuna wakati unaweza kumpigia simu akakwambia nipo bize kuna ishu naifanya kumbe miyeyusho tu, labda kalala zake anachati. Wasanii wengi wakubwa wanajipa ubize wasiokuwa nao. Kusema suala la kufanya kazi na msanii mdogo mi nadhani unaweza kufanya tuu kinachomata zaidi ni kazi nzuri." - Ommy alifunguka.
Msikilize hapa chini akifunguka