Ijumaa , 5th Jun , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Aziz Azion amemfukuza kazi aliyekuwa meneja wake ambaye anafahamika kwa jina Bashir, kwa tuhuma za ubadhirifu.

Aziz Azion

Kutoka katika chanzo cha kuaminika, Aziz amechukua hatua hiyo baada ya tukio la kumpatia pesa meneja huyo kwa ajili ya kazi ya kutangaza onesho lake lililokuwa lifanyike leo, ambapo Bashir alitumia pesa hizo kuwekeza katika biashara yake binafsi.

Hatua hiyo imepelekea kuzua ugomvi mkubwa kati ya msanii huyo na meneja wake ambapo mpaka sasa hawafanyi kazi tena pamoja.

Tags: