Jumanne , 27th Apr , 2021

Mpenzi na baba mtoto wa msanii Amber Lulu aitwaye Ember Botion amesema mtoto aliyempata na Amber Lulu ni wake mwenyewe na haukua ujauzito wa Uchebe au P Funk Majani kama ilivyokuwa inasemekana mitandaoni.

Msanii Amber Lulu na baba wa mtoto wake Ember Botion

Ember Botion amesema alikuwa na maswali mengi kipindi zinatoka taarifa zinazosemakana kwamba ujauzito huo ni wa Producer P Funk Majani na Uchebe, lakini Amber Lulu mwenyewe alimuaminisha kwamba ujauzito ni wake.

"Kuna muda ilikuwa inanipa maswali sana lakini nikimsikiliza yeye mwenyewe anasema ujauzito ni wangu kwa hiyo nikawa sina la kusema zaidi ya hivyo anavyoniaminisha mpaka amejifungua nimeona kweli, pia nataka watanzania wamuone kisha wamuangalie mtoto halafu waniangalie na mimi, haitaji DNA kwa sababu nina damu kali sana" ameeleza Ember Botion

Aidha amesema ifikapo siku 40 baada ya mtoto wao kuzaliwa ndiyo siku ambayo watu watapata nafasi ya kumuona na kumfanyia dua.