Alhamisi , 9th Jul , 2015

Meneja wa Tip Top Connection Babu Tale anatarajia kuwaalika watu katika futari maalum itakayoandaliwa siku ya Jumanne huko Tip Top eneo la Manzese maalum kwa ajili ya dua ya kuwakumbuka marehemu baba yake na kaka yake Abdu Bonge.

Meneja wa Tip Top Connection Babu Tale

Babu Tale pia ameweka wazi sababu ya yeye binafsi kuwa nje ya kundi katika kutoa ushirikiano wa kumsapoti msanii Diamond Platinumz kutokana na kile kinachosemekana kuwa amelisaliti kundi japokuwa yeye binafsi amesema kuwa hivi sasa anatarajia kufanya nyimbo ya kundi kwa kumshirikisha mkali huyo.