Jumamosi , 11th Apr , 2015

Barakah Da Prince, staa ambaye ameuanza mwaka 2015 vizuri na projekti yake ya Jichunge, ameweka wazi habari nyingine njema kwa mashabiki wake kuwa muziki wake umefunguka sasa.

Barakah Da Prince

Baraka amesema sasa anangalia nnje ya mipaka zaidi, akiwa katika mazungumzo na mastaa wakubwa kabisa Afrika, kuweka sawa mipango ya kolabo.

Barakah Da Prince kupitia eNewz pekee, akatoa list ya vichwa hivyo ambapo ndani yake yupo staa wa muziki Patorankin kutoka Nigeria, Jaguar kutoka Kenya na vilevile Chameleone kutoka Uganda.

Barakah Da Prince amesema kuwa, alianza muziki akiwa anaangalia mbele na mbali zaidi, na akiwa anatengeneza kazi sasa, anafahamu itakayofuata itakuwa vipi, kitu ambacho kinampanguvu ya kuwapatia mashabiki wake ahadi kuwa, ujio wake mpya na muziki wake kwa ujumla utaifikisha Bongo Flava mbali zaidi.

Patorankin