Ben Pol atafakari cha kumjibu Nay wa Mitego

Alhamisi , 6th Feb , 2020

Mkali wa RnB Bongo, Ben Pol, amepata kigugumizi cha dakika moja  kumjibu Nay Wa Mitego ambaye alimwambia kwamba amepata ganda la ndizi, amesahau muziki na ameolewa nchini Kenya, baada ya kumuona anakula sana bata.

Pichani kushoto ni Ben Pol, kulia Nay Wa Mitego

Nay wa Mitego amesema hivyo kupitia wimbo wake wa ipo sawa, baada ya Ben Pol kula bata sana nje ya nchi akiwa na mpenzi wake Anerlisa Muigai.

Kwa upande wa Ben Pol akijibu tuhuma hizo, ametafakari kwa muda kisha amejibu hana maneno mazuri ya kumwambia Nay Wa Mitego.

"Huwezi amini kwenye bata nililokula sio kama kuna mtu nataka kumkomoa au kutaka kumuonyesha mtu kitu chochote ni ukurasa wa maisha ambao umepita au upo ninaouishi,  cha umuhimu ni kwamba, hakuna dhuluma wala cha haramu au ushenzi wowote unaofanyika, kuhusu Nay wa Mitego mmmhh sina maneno mazuri kwenye hilo na sina cha kumwambia" ameeleza Ben Pol.

Ben Pol ni mmoja wa wasanii ambao wamesafiri na kula bata sana nje ya nchi mwaka 2019, baada ya kuwa kwenye mahusiano na mfanyabiashara maarufu nchini Kenya aitwaye Anerlisa Muigai.