Alhamisi , 30th Oct , 2014

Msanii wa muziki Ben Pol, amesema kuwa yeye huwa hana utaratibu wa kuzishindanisha rekodi zake anazotoa, kutokana na kila moja kutoka na uzito wake na mvuto wa tofauti na nyingine.

Ben Pol

Ben Pol amesema kuwa, kila ngoma yake huwa inajitengenezea mashabiki wake ambao huwa ni makundi tofauti, na hii ndio sababu yake ya kutokupenda kuzipambanisha kwa ukali wake.

Ben Pol ametoa maelezo haya kutokana na mtazamo wa mashabiki kuwa, kwa mwaka huu ngoma ya pekee ambayo imeweza kufanya poa zaidi ya nyingine zote alizotoa ni “Jikubali”.