Billnass afunguka alivyoachana na mpenzi wake

Alhamisi , 2nd Jul , 2020

Msanii Billnass amesema hajutii kitendo cha kurudiana na Nandy kwa sababu nguvu ya mapenzi ndiyo imewakutanisha tena pia haikuwa rahisi yeye kuachana na mpenzi wake ili kurudiana na Nandy.

Wapenzi pia ni wasanii Billnass na Nandy

Billnass amesema hawezi kuzielezea sababu zilizofanya kuachana na aliyekuwa naye ili kurudiana na Nandy ila ilitokea tu kuwa hivyo na hajutii kwa sababu yupo sehemu salama.

"Kabla ya bugana hakukuwa na mipango yoyote zaidi ya kuwa karibu na kufahamiana pia nguvu ya mapenzi na mapenzi ya kweli ndiyo yameturudisha, haikuwa rahisi kama niliamua kummwaga niliyekuwa naye ili nirudiane na Nandy siwezi kuelezea kwa harakaharaka ila ilitokea sababu ya kuwa hivyo na sijutii kwa kilichotokea najua nipo sehemu salama

Aidha Billnass amesema tangu amerudiana na Nandy wanajiona wamekuwa, pia tangu warudiane hawajawahi kukorofishana hadi inafikia hatua ana-miss kugombana na Nandy.

Zaidi tazama kwenye mahojiano kamili hapo chini