Jumatano , 21st Aug , 2019

Wasanii wa filamu za BongoMovie wakishirikiana na Miss Tanzania Elizabeth Makune, wamepanga kutengeneza filamu katika mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro.

Wasanii wa filamu

Wakizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya bodi ya utalii Tanzania mwenyekiti wa BongoMovie Steve Nyerere amesema, 

"Tunapenda kumshukuru Mh. Hamisi Kigwangalla kwa nafasi aliyotupa sisi wasanii, tunaenda kutengeneza filamu ambayo haijawahi kutokea katika mbuga za Serengeti na Ngorongoro, hili dodo tusiliache twendeni tukatengeneze filamu iliyo bora na tumsapoti Miss wetu". 

"Sisi kama wasanii hili ni jukumu letu na wajibu kwa sababu tukiangalia nchi kama Brazil inategemea uchumi wa utalii kwa unaweza kuona sekta ya utalii ilivyokuwa na umuhimu serikalini" Ben Kinyaiya.

Baadhi ya wasanii wengine waliokuwepo katika uzinduzi wa huo ni Dude, Johari, Ebitoke, Witness.

Uzinduzi kamili wa kampeni hiyo utaandelea siku ya tarehe 30 ya mwezi wa nane katika hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi wa uzinduzi huo atakuwa ni Waziri wa Utalii na Maliasili Mh.Hamisi Kigwangalla.