Jumatano , 16th Feb , 2022

Ni headlines za staa wa filamu Bongo Jacqueline Wolper, amefunguka suala la tabia ya watu kusifia mtu au kusemea mazuri yake akiwa tayari ameshafariki.

Picha ya msanii wa filamu Jacqueline Wolper

Kupitia mtandao wake wa Snapchat Wolper ameandika kwamba 

"Hivi mtu ukifa kwanini unakuwa star, yaani jamani mtu ungekuwa unapewa nafasi ya kuamka na kuona hao watu wamekupost na kuandika vya uchungu na kurudi kulala nahisi wengi nahisi wangeomba nafasi pia ya kuwapiga kwanza au kuwasuta, no way mnajua kusifia mtu akifa".