Jumanne , 9th Dec , 2014

Tanzania Bara leo imeadhimisha miaka 53 ya Uhuru wake kwa shamrashamra za aina yake zilizoambatana na burudani mbalimbali zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Tanzania Bara

Katika maadhimisho hayo, yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa kawaida pia kulikuwa na michezo ya halaiki, sarakasi, ngoma za asili kutoka katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.