Jumanne , 21st Apr , 2015

Staa wa muziki Jose Chameleone pamoja na Vampino kutoka nchini Uganda, wamegusa hisia za wengi kufuatia hatua yao ya kumaliza tofauti zao na kuwa kitu kimoja, hatua ambayo ni habari nyingine njema kwa tasnia ya muziki nchini Uganda.

wasanii wa nchini Uganda Chameleone na Vampino

Kitendo hicho kimefanyika mwishoni mwa wiki baada ya wawili hao kukutana katika kiwanja kimoja cha starehe huko Kampala, ambapo kutokana na umri, uzoefu na mtazamo mpya wa mambo sasa, hawakuona haja ya kuendeleza uhasama kati yao.

Kwa taarifa za chinichini kufuatia kupatana kwa mastaa hawa, kuna mpango pia wa kuwathibitishia hilo mashabiki kwa Vampino kuwa moja ya wasanii watakaohusika katika shoo ya Chameleone ya Wale Wale Double Trouble itakayofanyika huko Uganda May 1 mwaka huu.