
Chance ameandika ujumbe akitoa taarifa ya uamuzi huo kwenye ukurasa wake wa instagram, ambapo ameeleza namna ambavyo alikulia kwenye familia ya kidini, na kujuta kwake kwa kutofuata misingi hiyo ya kumjua Mungu zaidi.
Hatua hiyo imekuja wiki moja baada ya kuachia audio ya ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la 'The man who has everything'.
Hivi karibuni msanii huyo alitajwa kuwa na uhusiano na msanii mwenzake wa kiume, Jaden Smith, ambapo inadaiwa wawili hao walikuwa na uhusiano kwa kipindi kirefu lakini walikuwa wakifanya kwa siri.