Jumanne , 8th Sep , 2020

Wasanii wa Killy na Cheed ambao wamejiondoa kwenye lebo ya Kings Music ya Alikiba, wametangaza rasmi kusainiwa na lebo ya Konde Gang Music Worldwide ambayo inasimamiwa na msanii Harmonize.

Wasanii Killy na Cheed wakiwa na Harmonize baada ya kujiunga na Konde Gang

Wasanii hao wametangaza hilo kwa pamoja kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram, huku wakimshukuru boss wao wa zamani Alikiba kwa kuwaonyesha njia na kuwaamini kufanya nao kazi. 

"Siwezi kumsahau kaka angu aliyenilea, akaniamini na kunishika mkono na kuniaminisha zaidi kwa watanzania hasa kwa mashabiki wa BongoFlavour, na kunionyesha njia katika kipindi chote tulichokuwa pamoja kaka angu Alikiba

"Napenda kuwataarifu mashabiki zangu na watu wote wanaosupport kazi zangu kiujumla tangu hapo awali mpaka hapa nilipofikia, nawajulisha kuwa kijana wenu nimejiunga rasmi na kampuni ya uzalishaji na usimamizi wa muziki Tanzania Konde Gang" wameandika Killy na Cheed 

Cheed na Killy walijitoa Kings Music mwezi Aprili, hivyo wataungana na wasanii kama Ibrah Tz, Young Skales kwenye lebo ya Konde Gang ambayo inasimamiwa na Harmonize.