Chiddi Mapenzi amlilia mkewe wa zamani,Shamsa Ford

Jumatatu , 30th Mar , 2020

Unaambiwa umuhimu wa mtu hujitokeza pale unapompoteza, ndicho kinachomtokea mfanyabiashara wa mavazi Chiddi Mapenzi, baada ya kuachana na aliyekuwa mke wake Shamsa Ford.

Chiddi Mapenzi na Shamsa Ford siku ya harusi yao

 

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Chiddi Mapenzi ameweka ujumbe mzito kwa kueleza hatakuwa wa kwanza kulia kwenye mapenzi na anashindwa kujizua kwa kumkumbuka Shamsa Ford.

"Sitokuwa wa kwanza kulia kwenye mapenzi, nakukumbuka Shamsa nashindwa kujizuia vyote ulivyokuwa unanikataza kwa faida yangu mwenyewe ndiyo sasa hivi naviona, popote ulipo naomba ujue nakukumbuka sana mama, sina mtu wa kunipa moyo,sina rafiki kama wewe,wewe ndiyo msiri wangu,nakukumbuka mama na familia ni kila kitu dah" ameandika Chiddi Mapenzi.