Ijumaa , 25th Oct , 2019

Rapa Country Boy kupitia mahojiano aliyofanya na EATV & EA Radio Digital amesema kuwa "Life style" yake hamuigi msanii mkubwa wa HipHop duniani Lil Wayne japokuwa watu wanamsema sana kuhusu hilo.

Kushoto ni Country Boy na kulia ni Lil Wayne

Country Boy amesema anapenda sana kuvaa, kwenda na fashion ila anawatumia mastaa wakubwa kama Lil Wayne, Wiz Khalifa na Migos ila sio kama anawaiga kila kitu na kuzidisha uhalisia wake.

"Ni katika aina ya kujikubali na kujipenda nimekuwa nafatilia vitu vingi na napenda "fashion" na kuangalia ubunifu  wa watu wanavyovaa. Mimi navaa tofauti na watu wengi sana, huwa navaa vitu vinavyoitwa nyuki lazima vionekane. Watu ninaowafuatilia ni wanyamwezi sana kama Lil Wayne, Wiz Khalifa na Migos" ameeleza

Aidha akizungumzia kuhusu watu na mashabiki kumsema kuwa  anamuiga Lil Wayne hadi kupitiliza uhalisia wake Country Boy amesema 

"Nadhani aliyesema hivo alikuwa na mawazo ya kimaisha na akaamua kusema hivyo maani mimi najiona nimejipata katika uhalisia wangu labda wameniona pengine nina rasta, Lil Wayne anatumia "Auto tunes" mimi natumia sauti nyingine kabisa . Mashabiki wanataka wakutoe  kwenye njia ili umjibu" ameongeza.