Jumamosi , 19th Sep , 2015

Nusu fainali ya mashindano makubwa ya Dance 100% 2015, leo hii imekuwa ndio habari ya mjini ambapo makundi 10 yenye uwezo mkubwa wa kudansi wamekuwa na kibarua cha kushindanisha uwezo wao ili kuwezesha kupata makundi 5 bora zaidi yatakayoingia fainal

Dance 100% 2015

Ushindani mkali ambao haukuwahi kushuhudiwa juu ya jukwaa la kisasa kabisa umekuwa dhidi ya makundi yote ya Quality Boys, The WD, Cute Babies, The Best, Team Makorokocho, Team ya Shamba, Wazawa Crew, Best Boys Kaka Zao, Majokeri na The Winners Crew, wote hawa wakiwania nafasi 5 za kutinga fainali za michuano hiyo.

Mpambano huo ambao leo umefanyika kwa mizunguko miwili, unaendelea kuendeshwa kwa umakini mkubwa kabisa na kuamuliwa na majaji Super Nyamwela, Queen Darleen pamoja na Shetta wakiongezeka wawili wapya na kufanya jumla ya majaji katika hatua hii kufikia watano.

Baada ya mzunguko huo, sasa macho ni kwenye hatua ya fainali ambapo kitita cha fedha taslim shilingi milioni 5 za Tanzania ndio zawadi kubwa inayowaniwa, swali kubwa likibaki kuwa ni nani atakayeibuka mshindi wa kitita hicho.

Ni Burudani mwanzo mwisho, Dance 100% 2015.

Majaji wawili wapya walioongezeka