Dance 100%, usaili kukamilika J'pili

Jumatano , 30th Jul , 2014

Baada ya kumaliza usaili wake wa pili wa Dance100% 2014 pale Don Bosco Oysterbay Jumamosi, sasa imebaki nafasi moja tu ya mwisho kwa makundi yenye vipaji vya kudansi Tanzania.

Mashindano haya makubwa yamefikia hatua ya usaili wa mwisho utakaofanyika Temeke jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya TCC Chang'ombe Jumapili tarehe 3 mwezi Agosti.

Mpaka sasa makundi 10 tayari yamekwisha patikana ambapo yanaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali ya mashindano haya makubwa nchini Tanzania.

Mchongo mzima kuhusiana na kile kilichofanyika Oysterbay na kufanikisha kupatikana kwa makundi matano, utaruka hewani kupitia show kali ya Dance100% ambayo itakujia leo, kuanzia saa moja kamili jioni hapa hapa EATV.