Ijumaa , 22nd Aug , 2014

Mashindano makubwa ya kudansi Afrika Mashariki, Dance100% (2014) hatua ya robo fainali yatarajia kutikisa kiburudani hapo kesho Jijini Dar es salaam.

Mashindano ya kucheza muziki ya Dance100% 2014

Mashindano haya yatakayohusisha makundi 16 makali ya kudansi, yatafanyika kesho Jumamosi katika uwanja wa Oysterbay Don Bosco, na makundi yataanza kuonesha uwezo mbele ya majaji kuanzia saa 6 mchana.

Tukio hili linatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake hasa kutokana na ushindani na uwezo mkubwa wa makundi yote ambayo yanashiriki. Dance100% 2014 yanakwenda na swagga ya #2014Dance100%.

Tukutane Jumamosi hapo kesho katika uwanja wa Oysterbay Don Bosco jijini Dar es Salaam.