Dau la Mzee Yusuph baada ya kurudi kwenye Muziki

Jumatatu , 3rd Aug , 2020

Mkali wa muziki wa Taarab Mzee Yusuph amesema shida ndiyo zimemrudisha kwenye muziki na ili aweze kufanya show kwa anayemuhitaji gharama yake ni Shilingi Milioni 7 kwa Mkoa wa Dar Es Salaam tu.

Mzee Yusuph amesema hakuwa na mipango yoyote ya kurudi kwenye muziki ila imetokea kwa sababu tu, na hakuna mtu yeyote aliyemshauri kurudi kwenye muziki.

"Kuna mtu anayefanya kazi kwa sababu ya raha, kila mtu anafanya kazi kwa sababu ya shida atataka kula au kulala, shida ndiyo inafanya sisi tuishi na tupigane, kama kuna mwenye raha halafu abaki nyumbani mwancheni alale tuone kama hatoondoka, hata ukiwa na mke huna chakumpa nayo ni shida hiyo" amesema Mzee Yusuph

"Kama kuna mtu ananitaka mwenye ukumbi wake kama anataka kunichukua labda awe na watu zaidi ya mia tano maana mimi pesa yangu ni kubwa , dau langu linaanzia Milioni 7 kwa mkoa wa Dar Es Salaam , zipo zingine hadi za Milioni 10 hadi 15" ameongeza

Zaidi tazama kwenye mahojiano kamili hapa chini.