Jumatatu , 12th Dec , 2016

Kusinda tuzo ya muigizaji bora wa kike katika Tuzo za EATV kumemtoa machozi Chuchu Hansy na kumkumbusha siku aliyovunja ungo huku akiwashukuru mashabiki wake waote waliompigia kura.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chuchu amesema ushindi huo umemfanya akumbuke maneno aliyokuwa akipewa na mama yake katika kipindi cha ukuaji wake kuwa anapaswa kumuheshimu kila mtu bila ubaguzi ili afanikiwe kimaisha, na hilo ndilo ambalo amekuwa akilifanya siku zote huku akiamini kuwa hiyo ndiyo siri ya yeye kuibuka kinara katika waigizaji wote wa kike nchini Tanzania.

Chuchu amezipongeza tuzo hizo pamoja na kuwataka mashabiki wake kuendelea kuwa naye bega kwa baga.

Hiki ndicho alichoandika.

Meneja wa Chuchu Hansy (Kulia) akiwa ametinga stejini huku akiwa ndani ya taulo kwa niaba ya Chuchu ambaye hakuwepo
Tags: