Jumatano , 30th Dec , 2015

Diva anayefanya poa katika tasnia ya filamu na muziki nchini Baby Madaha ambaye amepata ajali ya kuteguka enka mguu wake wa kulia amesema kuwa hali yake hiyo haitomzuia kukamilisha kazi zake za muziki na filamu.

msanii wa muziki na muigizaji filamu nchini Baby Madaha

Baby J ameongea na enewz kuwa japo kwa upande wa sekta ya soko la filamu nchini limekuwa likisuasua, ila ameshukuru kuwa amepata mafanikio yake kupitia muziki na amejiandaa kuzindua filamu yake iitwayo 'Saint and Ghost pamoja na kampuni yake.