Exclusive : Lulu Diva ampigia simu Jaguar

Jumatatu , 13th Jan , 2020

Kupitia EATV & EA Radio Digital, tumekuandalia mahojiano maalum kati ya Lulu Diva, ambaye  amempigia simu msanii na Mbunge wa jimbo la Starehe kutoka nchini Kenya Jaguar ili kuzungumzia suala la mahusiano yao kwa sasa.

Pichani ni Lulu Diva na Jaguar

Lulu Diva amefikia hatua hiyo ya kumpigia simu Jaguar, baada ya kuulizwa mara ya mwisho kumtembelea Jaguar ilikuwa ni lini ambapo amesema,

"Mara ya mwisho sikumbuki maana sijaonana naye muda kidogo na sijaenda kumuona, nilikuwa nipo safarini kwa ajili ya kazi zangu, nimemkumbuka rafiki yangu ngoja nimpigie kama atapokea na asipopokea basi" amesema.

Baada ya kupiga simu hiyo ikapokelewa na Jaguar mwenyewe na akafunguka issue ya mahusianio yao kwa kusema.
"Nitakuja kutembea tu maana nawapenda sana watanzania , kama amekana itabidi nilifanyie maamuzi kuhusu hili ni msichana mrembo, hakuna mwanaume ambaye atamkataa Lulu Diva, siwezi kusema hewani kama namtaka ila ni msichana mrembo, mchapakazi na ana kipaji" ameeleza Jaguar.