
Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 walipotembelea EATV, leo
Hayo yamesemwa na Afisa Habari Kamati ya Miss Tanzania mwaka 2016 Hidan Ricco wakati wa ziara ya mafunzo kwa warembo hao iliyofanyika leo katika vyombo vya habari vya IPP ambao pia ni wadhamini wa shindano hilo.
Washiriki hao tayari wameingia kambini kwa ajili ya kuanza safari ya kulisaka taji lla Miss Tanzania 2016 katika shindano hilo lenye msisimko wa aina yake.
“Kwa mara ya kwanza shindano hili linafanyika Jijini Mwanza na hii ni kutokana na mahitaji ya wadau ambapo kwa kukidhi malengo yao tumeona ni vyema tuzingatie maoni yao ili kuboresha shindano letu ndiyo maana tunaanza na Mwanza” Amesema Ricco.
Kwa mujibu wa Ricco washiriki wa shindano hilo ambao wamepatikana kwa mchujo uliofanyika mikoani watakuwa na semina na ziara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja Dodoma, Singida, Geita na Mwanza ili kuweza kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Tanzania.
Shindano hilo tayari limeanza kwa washiriki kuwa kambini kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 29 fainali itakapofanyika Jijini Mwanza na mshindi kutangazwa.