Jumatatu , 11th Jan , 2016

Staa wa muziki H-Baba ametoa kauli ya kuwabeza wasanii wenzake, akieleza kuwa kwa sasa yupo kimya akiangalia mchezo kama baba mwenye nyumba ambaye akirejea, wasanii wengine kama wapangaji lazima waelewe juu ya uwepo wake.

Staa wa muziki nchini H-Baba

H-Baba ambaye majukumu ya kifamilia ambayo sasa ni makubwa si chanzo cha ukimya wake kwa mujibu wake, ameeleza kuwa nafasi yake ina maamuzi ya kuhamisha nafasi za wengine, na kila mtu ataelewa namna ambavyo ataufungua mwaka huu kama ambavyo anazungumza hapa.