H Baba aomba aoneshwe talaka

Alhamisi , 9th Jan , 2020

Msanii na mkali wa kukata mauno Bongo, H Baba amesema kama mke wake Florah Mvungi huwa anawaambia watu kwamba wameachana basi aoneshe talaka.

Kushoto pichani ni H-Baba, kulia ni Florah Mvungi

Akizungumza na eNewz ya East Africa Television, ambayo inaruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 jioni, na kumuonya mkewe huyo kuchunga kauli zake.

"Yule ni mke amenizalia watoto wawili, namuheshimu sana, ila achunge mahojiano yake anayofanya kwa sababu yanamdhalilisha yeye kama mama watoto, unajua ukiwa mke unatakiwa uwe bora usikurupuke" amesema H Baba.

Aidha H Baba ameongeza kuwa "Yule ni mke, mama wa watoto wawili, anatakiwa ajisheshimu na kulinda maneno kwa ajili ya watoto, kama kuna neno likija lizue lisitoke kwa sababu ya faida za baadaye, halafu sisi sio wapenzi ni mke na mume kama anawaambia mahusiano yamekufa awaoneshe talaka".

Pia H Baba amesema hana shida na Florah Mvungi ila anachoangalia ni watoto wake kwa sababu hata kwenye muziki alipumzika kwa miaka 5 kwa sababu ya kuwalea.