Ijumaa , 18th Sep , 2020

Msanii wa BongoFleva Lameck Ditto amekataa uwepo wa urafiki wa jinsia mbili tofauti ambao unawahusu mwanaume na mwanamke huku akidai kuwa urafiki wa hivyo lazima uwe na hisia ndani yake au jambo katikati yao.

Msanii wa BongoFleva Ditto

Akifafanua hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio, msanii Ditto amesema kuwa  yeye kama mwanaume anaelewa nini kinakachofuata au kitakachotokea mwisho wa urafiki huo.

"Ndani ya urafiki wa mwanaume na mwanamke  lazima kuna Jambo limejificha sijawahi kuona na kama wapo marafiki basi ni mmoja duniani tusidanganyane mimi ni mwanaume naelewa wanaume hatuwezi labda wanawake wanaweza vumilia urafiki ila sisi wanaume hatuwezi" amesema Ditto 

Aidha Ditto ameendelea kusema "Mwanaume lijali lazima apate hisia hata kama mtakuwa ni marafiki, kuna muda hisia zinakuja asikudanganye mtu urafiki wa jinsia mbili haupo"