Jumanne , 18th Apr , 2017

Muongozaji wa video  za muziki nchini ambaye kwa sasa ameshika chati Bongo,  Hanscana amefunguka na kudai kuwa kutegemea kukopi vitu vya kutoka nje ya Bongo kama vile nchi za Afrika kusini ni kuua ajira za watu wengi wa Afrika Mashariki.

Hanscana

Hascana kupitia ukurasa wake Instagram amefungukia hayo akiwa ameweka picha yake na msanii Eddy Kenzo kutoka Uganda na kudai kukopi kazi za watu wa Magharibi na Kusini ni kupoteza utambulisho wa sanaa ya Afrika Mashariki hivyo kutoa ahadi ya kupigania.

''Nitahakikisha game ya Afrika Mashariki inafika mbali zaidi kupitia muziki wetu wenyewe pamoja na video zinazozalishwa hapa hapa nyumbani Afrika Mashariki na waandaji wa hapa hapa E.A, Ili sanaa yetu izidi kujitosheleza ( kujitegemea zaidi ) na siyo mpaka tukakopi vitu toka Kusini ya mbali ama umagharibi na kupelekea kupoteza 'Id' yetu kisanaa na mbaya zaidi kuua ajira za vijana lukuki wanaotegemea sanaa hii dancers, models, make up artist, designers, producers ETC nina amini sana katika sisi"- Hanscana aliandika