
Harmonize (kulia) na Abella (kushoto)
Harmonize akiwa nje ya nchi jana Januari 2, 2021, alitangaza kutafuta mwimbaji wa kike ili amshirikishe kwenye ngoma yake hiyo na baada ya mapendekezo ya watu alitangaza kumtafuta mwimbaji wa nyimbo za kurudia 'Cover', aitwaye Abella na alifanikiwa kumpata.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amethibitsha kuwa amerejea nchini leo na usiku anakutana na Abella kwaajili ya kurekodi audio ya wimbo huo.
Abella ambaye ana ulemavu wa mguu amejizolea umaarufu mtandaoni kwa kurudia nyimbo za wasanii mbalimbali huku wengi wakisifia uwezo wake mkubwa pamoja na sauti ya kuvutia.