
Picha za wasanii kushoto AT, kulia ni Tausi
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, AT amesema urefu ulimletea madhara kwani alikuwa anajigonga kwenye mlango wa Bibi yake ambao ulikuwa mfupi, ila hajawahi kukosa mpenzi kutokana na urefu wake.
"Hakuna shida ambayo nimeipata wakati narefuka kama kujigonga sana kichwani kwenye mlango wa bibi yangu ambao ulikuwa ni mfupi, ila kuhusu wanawake wanapenda sana wanaume warefu wenyewe wakikaa wanaongea kabisa kuwa mtu mrefu anawapendeza, kwa mfano Tausi amesema yeye ni mfupi hataki mwanaume mfupi, urefu ni dili" ameeleza AT.
Aidha AT ameendelea kusema hajawahi kukosa kitu cha maana kwa sababu ya urefu wake labda ni suruali tu kuwa fupi kwake, pia anaufurahia urefu wake ambao amejaaliwa na Mungu na hata watoto wake ni warefu pia.