
kundi la muziki kutoka South Afrika Mafikizolo
Wakizungumza na Enewz Mafikizolo wamesema kuwa kwa wasanii wanaohitaji kolabo na kundi lao wao hawaangalii ukubwa wa jina la msanii bali wanachokiangalia radha ya msanii na uwezo wa mtu katika kuimba.
“Huwa hatuangalii jina la msanii sisi tukipenda tu radha ya msanii tunafanya nae kolabo na hivyo ndivyo wasanii wengine wanapaswa kuviangalia”,walisema Mafikizolo.
Huku wakitolea mfano walivyowapa nafasi uhuru na Maphorisa na kuwaweka juu katika ramani ya muziki wakati walikuwa hawatambuliki katika game ya muziki lakini wao waliweza kuwafanya wao kutambulika na wengine kuanza kuomba kolabo kwao.