Akizungumza na www.eatv.tv Wastara amesema kwamba kitendo cha watu kumfikiria vibaya kinamtia uchungu na kinamvunja moyo, kwani ukizingatia hakuomba kupata matatizo aliyopata, na kwamba picha aliyopost ni ya muda mrefu akiwa nchini India.
“Kwa kweli inasikitisha na inavunja moyo sana kama Mtanzania, na kama mtu ambaye nina haki zote kama wengine, hii ni picha ambayo niliipiga wakati nipo India, na nafikiri nilieleza pia nilikuwa na matatizo ya kichwa, kwa hiyo ni moja ya kipimo na matibabu pia, kwa hiyo hiyo picha ni ya zamani wakati nipo India”, amesema Wastara.
Wastara amesema kwa sasa anaendelea vizuri na matibabu na hakuna tatizo linalomsumbua, hivyo watu wasitilie maanani maneno ya watu wanaomsema mabaya ili aonekane mbaya kwa jamii.