Ijumaa , 13th Sep , 2019

Staa wa mitandao ya kijamii na mjasiriamali nchini Kenya Huddah Monroe'Huddah The Bosschik' amewashutumu viongozi na mastaa kwa kugeuza siasa kuwa sarakasi nchini humo.

Huddah Monroe

Ameeleza hayo baada ya viongozi na baadhi ya mastaa kugombania nafasi ya ubunge katika kaunti ya Kibra iliyoachwa na Ken Okoth ambaye amefariki dunia.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Huddah Monroe ameandika “watu wamefanya mzaha, utani, chale, sarakasi na vichekesho katika kiti cha ubunge kaunti ya Kibra, mnahitaji kumpa kura zenu Octopizzo ambaye amezaliwa na amekuwa hapo anajua matatizo yanayoyakuta jamii”.

Kuhusu viongozi na mastaa wanaoitaka nafasi hiyo Hudda ameseama, "kuna bangi inasambazwa jijini Nairobi, hakuna atakayesema wanachotaka kufanya na dunia nzima inajua kibra ndipo kuna makazi duni ya watu ila wanafikiria kuja na kuaondoka muda wowote"

Pia amesema anachukia siasa kwa sababu viongozi wanawaachia watu ujinga na kwamba  anatamani awahamasishe vijana kwa yeyote atakayeleta siasa wampige mawe.

Mastaa ambao wanagombania kaunti hiyo ni wasanii wa Hip Hop, Prezzo na Octopizzo pamoja na mchezaji wa zamani wa taifa hilo na klabu ya Inter Milan aitwaye McDonald Mariga.