Idris apewa sharti hili kurudiana na Wema Sepetu

Jumatano , 25th Mar , 2020

Msanii Lulu Diva amesema Idris Sultan na Wema Sepetu, walikuwa wanapendana kweli na atafurahia kuona wamerudiana ila kwa njia tofauti ambayo ni kuweka mahusiano yao yawe ya siri.

Idris Sultan na Wema Sepetu

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Lulu Diva ambaye ni ndugu wa Idris Sultan amesema, mapenzi ya kweli huwa hayaishagi.

"Idris na Wema wanawasilina na wanaongea na siku zote mnapoachana sio lazima muwe maadui na mapenzi ya kweli huwa hayaishagi, wale watu walikuwa wanapenda sana, nitafurahia kuona wamerudiana ila kwa hali ya utofauti na mara ya kwanza" amesema Lulu Diva.

Aidha msanii huyo ameongeza kusema "Kama watarudiana tena au akiwa na mahusiano na mwanamke yeyote yule nisingependa kumuona mapenzi yake yakiwa hadharani kama mwanzo, nataka mapenzi yao yawe siri"

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.