Jumatano , 1st Apr , 2015

Kampeni ya ZamuYako2015 inaendelea kuwagusa wasanii mbalimbali huku wengi wakiendelea kuwahamasisha vijana kujiandikisha na kushiriki kupiga kura.

Msanii wa muziki wa Bongofleva Imma Nani

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Imma Nani amesema hii ni moja ya kampeni kubwa ambazo inambidi kijana kujitambua kuwa kura yake ndio inayoweza kuleta mabadiliko na sio tu kukaa vijiweni kulumbana na baadae kujutia viongozi wabovu wanaotokana na sisi wenyewe kudharau zoezi hili zima.

Aidha, mkali huyo aliyetoa video yake mpya iliyozinduliwa hivi karibuni hapa EATV aliyoibatiza jina 'Ni Wako' amesema kuwa hii ni moja ya kazi yake mpya ya kuufungua mwaka iliyoongozwa na Hascana ambapo akagusia pia mipango ya kutoa kazi na wasanii Belle 9, AY na pia GNako.