Irene Uwoya atoa siri ya kuitwa 'sister'

Jumatatu , 13th Mei , 2019

Mlimbwende kutoka kiwanda cha bongo movie, Irene Uwoya ameibuka na kutaja asiri yake ambayo hajawahi kuisema kwamba, alipokuwa akisoma sekondari alikuwa akivaa sketi ndefu mpaka chini kitendo kilichosababisha wanafunzi wenzie wampe jina la sista.

Irene Uwoya.

Uwoya amesema kuwa wakati ameanza kidato cha kwanza alikuwa mpole sana, wazazi wake wakamshonea sketi za shule ndefu mpaka mguuni kiasi ambacho wenzie walikuwa wakimtania na kumuita sista na kwa wakati huo alikuwa akiona kawaida tu. 

Yaani huwezi amini mtu akiniletea zile sketi leo naweza nisimuelewe kabisa na nitamshangaa sana, lakini mimi nilikuwa nazivaa wenzangu wananitania na kuniita Sista Irene", amesema Uwoya.

Uwoya amekuwa akiingia katika malumbano na mashabiki wake kutokana na uvaaji wake wa nguo fupi.