Isabella akiri kumpenda kaka wa Godzilla

Jumanne , 5th Mar , 2019

Baada ya kaka yake Godzilla kusema hawamtambui Isabella Mpanda kama mpenzi wa marehemu Godzila na kumtaka kuacha kumtafutia mdogo wake skendo ambazo hakuwa nazo, Bella amesema anampenda shemeji yake.

Isabella

Akiongea kupitia eNEWZ Bella amesema kwamba hakuwa akimfahamu kaka yake na Zilla na wala hawakuwahi kukutana hata siku moja kwa kuwa alikuwa anakaa nje ya Dar es Salaama japo baada ya kumzika Zilla kaka yake alienda nyumbani kwa Bella na wakapata kuongea mambo machache ambayo Bella hakutaka kuyaweka wazi.

"Mimi nampenda sana Shemeji yangu na kwa kweli nitampenda mpaka mwisho wa maisha yetu ya hapa duniani sikuwa namfahamu na wala sikuwahi kukutana naye kabla ya msiba wa Zilla ila baada ya kumzika Zila alinitafuta na tukaongea naye mambo yetu wenyewe ambayo sitaweza kuyasema hapa zaidi ya kusema tu nampenda sana shemeji yangu", aliongea Bella.

Miss Bella Pia anasema kuwa kundi la Scorpion Girls hawapendani ndio maana wameshindwa kurudisha kundi hilo japo anasema hawezi kusema limekufa maana huenda wakaja wakarudiana na kutoa nyimbo ya pamoja japo kwa sasa yeye ameamua kutoa nyimbo zake mwenyewe na atakuwa anatoa nyimbo hizo mara kwa mara na sio kama zamani.

Bofya hapa chini kutazama zaidi.