Isha Mashauzi adai kuwa yeye sio mtu wa kudanga

Jumanne , 3rd Dec , 2019

Muimbaji wa muziki wa Taarabu hapa nchini, Isha Mashauzi, ameeleza siri ambayo watu wengi hawaijui kutoka kwake, ambapo amesema hata kama hana pesa lakini familia yake haiwezi kulala njaa na wala hajawahi kudanga.

Picha ya msanii Isha Mashauzi.

Isha Mashauzi ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, kwa kusema moja ya kitu ambacho ameachiwa na Mama yake ni kuishi na watu vizuri na ndicho kinamsaidia hadi sasa.

"Mimi ni mtu mkarimu sana, mcheshi na mzuri kwa watu wangu ambao wananijua na wale wa karibu na mimi wanaelewa hilo, ila ni kichefuchefu ukinivuruga muda wowote navurugika tu naendana na vile unavyotaka wewe kama maji tu yakienda huku naenda yakirudi pia narudi" amesema Isha Mashauzi.

Aidha Isha Mashauzi ameongeza kuwa "Kama utakuwa rafiki mwema kwangu utafurahia urafiki wetu, kama ukiwa mbaya utachukia tu na hatutaendana, kwa sababu mimi sio mtu wa kudanga au kujichetua, napenda upole, kuishi na watu vizuri, kuna muda hata nyumbani kwangu naweza nisiwe na pesa ila watoto wangu wanakula yote ni kuishi na watu vizuri".