Jackline Wolper aingia msikitini kuswali

Ijumaa , 11th Jan , 2019

Muigizaji wa 'Bongo Movies', Jackline Wolper ameweka wazi kuwa kwa sasa anaswali msikitini, jambo ambalo limeonekana kushangaza.

Inafahamika kuwa Wolper ni Mkristo na hivi karibuni aliweka wazi kuwa ameokoka, lakini baada ya mwandishi wa www.eatv.tv kumtafuta kwaajili ya mahojiano akajibu kuwa anaingia msikitini saa 6 mchana kuswali swala ya Ijumaa.

Awali mwandishi wa habari hii alimpigia kutaka kujua juu ya 'post' aliyoweka katika mtandao wa instagram inayoelezea kuwa yupo kwenye mahusiano mapya, ndipo alipomuomba dharula mwandishi na kusema kwamba anaingia msikitini kwenye ibada, kisha atamtafuta wazungumze kiundani.

“Nilipost kwa sababu alinifurahisha, nikaona niandike hivyo, ila samahani naingia msikitini kuswali, nikitoka nitakupigia tutazungumza kiundani”, amesema Jackline Wolper.

Kutokana na kauli hiyo mpaka sasa bado haijafahamika wazi kama msanii huyo ambaye alishawhai kubadili dini kwa sababu ya mapenzi, amerudi tena kwenye Uislamu ama la, kwani siku za hivi karibuni amekuwa akionekana kupenda kujifunga ushungi, na hata siku ya 'birtday' yake aliita wanafunzi wa madrasa na kumsomea dua, kitendo ambacho hakifanani na imani yake ya Kikristo inayofahamika.