Jumanne , 5th Jan , 2016

Nyota wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya, ameamua kuanza mwaka 2016 na mikakati mipya katika jukumu lake kupambana na tatizo la ulevi na dawa za kulevya Kenya, kukiwa na rekodi ya kukua kwa kasi kwa idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya.

Nyota wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya

Jaguar ameeleza kuwa, inashtusha sana kutambua kuwa asilimia 50, yaani nusu ya vijana Kenya wameathirika na dawa za kulevya, akisisitiza kuwepo na haja ya kuchukuliwa kwa hatua za juu zaidi zikihusisha kila mwananchi kupambana na tatizo hilo.

Kwa mwaka jana msanii huyo amekuwa akipambana pia na watendaji na mfumo mbovu wa mamlaka ya kupambana na ulevi na dawa za kulevya nchini humo NACADA, akiwa kama mjumbe wa bodi ya viongozi, mwaka huu mpya akiwa na malengo ya kupambana zaidi kuwaokoa vijana dhidi ya janga hilo.