Jumatatu , 30th Jun , 2014

Msanii wa muziki Lady Jay Dee ametangaza kuwa ziarani katika sehemu mbalimbali, ambapo kwa kuanzia amekuwa huko Kenya kwa ajili ya show na pia kolabo na wasanii kadhaa nchini humo.

Mwimbaji Lady Jaydee

Jaydee aka Anaconda alipagawisha mashabiki huku akichangia jukwaa moja na nyota wakubwa Afrika Mashariki akiwepo Ken wa Maria, Radio na Weasel wa Uganda, Wyre pamoja na Kidumu.

Baada ya tukio hili kubwa Lady Jay Dee ametangaza kuwepo safarini kwa shughuli zake, mpaka mwezi Agosti ambapo ameahidi kuwafahamisha mashabiki wake kila kinachoendelea kumhusu kupitia kipindi chake cha Diary ya Lady Jay Dee kinachoruka hapa hapa EATV.

Hii inakuwa ni hatua nyingine kubwa kwa sanaa ya Lady Jay Dee kwa mwaka huu akiwa sasa anatamba katika chati mbalimbali kupitia wimbo wake unaokwenda kwa jina “Nasimama”.