Jumanne , 4th Aug , 2015

Mtayarishaji muziki wa kimataifa kutoka Comoro, Joh Banjo ambaye kwa sasa yupo hapa nchini kikazi, ameshukuru watanzania kwa kuelewa kile anachofanya, hasa baada ya mafanikio makubwa ya rekodi alizofanya na wasanii wa hapa.

Mtayarishaji muziki wa kimataifa kutoka Comoro, Joh Banjo

Joh Banjo ambaye pia ni mwimbaji mzuri, ameeleza pia kukua na kukubalika kwa Bongo Flava, sio tu ndani ya Comoro bali Afrika nzima, akiahidi kutengeneza muunganiko wa kazi na ladha ambayo itang'arisha muziki huo na kuupeleka mbali zaidi.